• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

MIAKA 61 YA UHURU WATANZANIA WAJIKITE KATIKA MAENDELEO- DC MOYO

Posted on: December 9th, 2022

Ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara yenye kauli mbiu “Amani na Umoja ni nguzo ya Maedeleo yetu” Wilaya ya Iringa imefanya kongamano la kujadili Maendeleo ya miaka 61 ya Uhuru leo 9 Disemba 2022 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo Manispaa ya Iringa.

Akizungumza katia kongamano hilo Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Mohamed Moyo amesema kuwa  tulipo toka na tulipo sasa hivi kama nchi tumepiga hatua kubwa sana kwa kuwa Sekta zote za ,kiuchumi, na kijamii kuna mabadiliko makubwa hususani kwa mtu mmoja mmoja.

Moyo amesema kuwa ni lazima watanzania wajikite katika maendeleo ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini lakini bila kusahau uzalendo kwa kuwa ndio kitu kikubwa.

Awali akiwasilisha mada katika kongamano hilo Mhadhiri kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii CDTI Musa Rashid amesema kama Nchi mpaka sasa imefanikiwa kuhakikisha inapambana na ujinga umasikini na maradhi kwa kuanzisha shule,,kufungua vituo vya Afya na kutoa Mikopo isiyo na riba kwa  wananchi kwa lengo la kuwainua kiuchumi

“Tumefanikiwa kupambana na ujinga kwa kuwa shule zimejengwa kila sehemu hakuna mahali ambapo hakuna shule hilo limetusaidia kupiga hatua kwenye Sekta ya Elimu”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kupinga ukatili Mkoa wa Iringa nduguu Silvano Ernest amesema kuwa kupitia Maadhimisho hayo ya miaka 61 ya Uhuru yaende sambamba na kupinga ukatili kwa watoto  na wanawake ili kukomesha matendo hayo katika jamii yetu.

Naye mwananfunzi kutoka Chuo Kikuu cha Katholiki ( RUCU) ndg.Desmond Laurent amesema kuna haja ya kuendelea kuwa na makongamano kama hayo kwakuwa yanaendelea kutukumbusha watanzania thamani ya kuendelea kulinda Uhuru wa Taifa letu.

Mada zilizowasilishwa katika kongamano hilo  ni Maendeleo endelevu ya Elimu,Maendeleo ya jamii katika nyanja zote,,uzalendo na mchango wa viongozi katika harakati za ukombozi.

Akifunga kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amewataka  watanzania wote kuendelea kudumisha uhuru  na kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kwani hiyo ndiyo zawadi pekee tuliyopewa na waasisi wa Taifa letu.

Aidha Mhe Moyo  amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia vibaya jukwaa la kisiasa kuwagawa watanzania na kuwataka watanzania wasikubali kugawanywa.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa dini,viongozi wa chama na Serikali,wakuu wa sehemu na Vitengo,watumishi,wanafunzi wa shule za Msingi,Sekondari,vyuo vya kati na vyuo vikuu ambapo awali katika wiki ya maadhimisho hayo shughuli mbali mbali za kijamii zilifanyika.

Shughuli zilizofanyika ni kupanda miti katika shule ya Sekondari ya Mawelewele ,Hospitali ya wilaya ya Frelimo.kufanya usafi na kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa,Mabonanza ya michezo na mashindano ya Insha katika Shule za Msingi na Sekondari ambapo washindi walikabidhiwa zawadi na Mgeni rasmi katka kilele cha Maadhimisho hayo.

K/Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaa, Iringa.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022 - MANISPAA YA IRINGA December 11, 2022
  • TANGAZO MUHIMU.. January 02, 2023
  • TANGAZO MUHIMU... January 09, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA VYUMBA VYA BIASHARA KATIKA STENDI YA IGUMBILO March 10, 2022
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • MNEC ASAS KUTOA MIL.100 KWA MACHINGA MANISPAA YA IRINGA

    March 14, 2023
  • BILION 1.9 KUKAMILISHA MACHINJIO NGELEWALA-MEYA NGWADA

    February 08, 2023
  • DKT. LINDA AAPISHWA DC MUFINDI

    February 03, 2023
  • RC DENDEGO AWAAGIZA MENEJA WA TANROADS NA TARURA KUONGEZA USMAMIZI NA UFATILIAJI KWA WAKANDARASI

    January 10, 2023
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa