TANGAZO
SERIKALI KUPITIA WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA) INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MANISPAA YA IRINGA KUWA HUDUMA ZA USAJILI NA UTOAJI WA VYETI VYA VIFO SASA INAPATIKANA KATIKA OFISI ZA KATA PAMOJA NA VITUO VYA TIBA NDANI YA MANISPAA YA IRINGA.
AIDHA ILI KUPATA CHETI HICHO, WANANCHI WOTE MNATAKIWA KUWA NA TAARIFA KAMILI ZA MAREHEMU IKIWEMO:-
JINA KAMILI
TAREHE YA KIFO
TAREHE YA KUZALIWA
ENEO LA MAKAZI
NA SABABU YA KIFO
RITHA SASA WAMEKUSOGEZEA HUDUMA HII MPAKA NGAZI YA KATA. KUMBUKA CHETI CHA KIFO HAKINA UKOMO WA MATUMIZI.
CHETI CHA KIFO NJIA BORA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU NA KUSAIDIA WATEGEMEZI KUPATA HAKI KISHERIA ZA KURITHI.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: mkurugenzi@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa